1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi na Ukraine zashambuliana kwa droni usiku kucha

Angela Mdungu
15 Septemba 2024

Urusi na Ukraine zimeendeleza kushambuliana usiku kucha. Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema Jumapili kuwa, imezidungua ndege 29 zisizo na rubani za Ukraine zilizorushwa kuilenga mikoa yake saba.

https://p.dw.com/p/4kdgc
Ndege isiyo na rubani ya Urusi
Muonekano wa droni ya Urusi chapa FPV KamikazePicha: Alexander Reka/ITAR-TASS/IMAGO

Kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram, wizara hiyo imeeleza kwamba  droni 15 kati ya 29 zilidunguliwa kwenye mkoa wa Byansk unaopakana na Ukraine wakati zilizosalia ziliharibiwa katika mikoa ya Smolensk, Orlov, Belgorod, Kaluga na Rostov.

Soma zaidi:Urusi yaishambulia Ukraine kwa droni usiku kucha 

Katika hatua nyingine, Ukraine nayo imearifu kuwa jeshi lake la anga limeziangamiza droni 10 kati ya 14 zilizorushwa na Urusi usiku wa kuamkia leo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Moscow ilirusha makombora mawili ya masafa marefu  yaliyoulenga mji wa bandari wa Odesa. Kulingana na mamlaka za mkoa huo, watu wawili wameuwawa kutokana na mashambulizi kwenye mji huo.