1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi, Iran hazikualikwa Mkutano wa Usalama wa Munich

7 Februari 2024

Urusi na Iran hazijaalikwa katika mkutano wa usalama wa mwaka huu mjini Munich, Ujerumani, baada ya waandaaji kudai kuwa mataifa hayo mawili hayaonekani kuwa tayari kushiriki mazugumzo juu ya usalama ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4c8d2
Christoph Heusgen, Mwenyekiti wa Mkutano wa Usalama wa Munich.
Christoph Heusgen, Mwenyekiti wa Mkutano wa Usalama wa Munich.Picha: DW

Mwenyekiti wa mkutano huo wa kila mwaka, Christoph Heusgen, amesema maafisa wa mataifa hayo hawajapata mwaliko kwa kuwa wanaonekana kutokuwa tayari kwa mazungumzo yenye tija.

Soma zaidi: Iran: Mazungumzo ya nyuklia yamefikia hatua muhimu

Mkutano huo ambao kwa kawaida huhudhuriwa na wakuu wa usalama na ulinzi duniani na ambao wakati mwengine huitwa "Mkutano wa Davos wa Ulinzi" utafanyika kati ya Februari 16 hadi 18 katika mji wa Munich ulioko kusini mwa Ujerumani.

Soma zaidi: Nchi za Magharibi zaonyesha mshikamano huku Urusi ikianza mazoezi ya nyuklia

Mkutano huo utafunguliwa siku chache kabla maadhimisho ya miaka miwili tangu Urusi kuivamia Ukraine na miezi minne baada ya vita vya Israel dhidi ya Hamas.

Heusgen amesema anatarajia maafisa waandamizi wa Israel wahudhurie mkutano huo.