Urusi imefanya mashambulio makubwa dhidi ya Ukraine
21 Januari 2025Matangazo
Jeshi la Ukraine limesema kwamba limefanikiwa kudungua droni 72 huku nyingine 59 zikitoweka kabla ya kufikia maeneo iliyolenga kuyashambulia.
Kikosi hicho cha anga cha Ukraine kimesema, kwamba baadhi ya majengo yaliharibiwa na mashambulio hayo kwenye mikoa miwili ya Ukraine lakini hakuna vifo vilivyotokea.
Urusi,Ukraine zashambuliana kwa droni usiku kucha
Kwa upande mwingine jeshi la Ukraine limesema limeshambulia miundo mbinu ya Urusi ya kiwanda cha utengenezaji ndege kwenye eneo la Smolensk, pamoja na kituo cha mafuta katika mkoa wa Voronezh.