1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZimbabwe

Upinzani Zimbabwe wazindua kampeni ya uchaguzi wa Agosti

17 Julai 2023

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa ameahidi kuustawisha uchumi na kuumaliza ufisadi, wakati alipoizindua kampeni ya chama cha Citizens Coalition for Change, CCC.

https://p.dw.com/p/4TzKW

Chamisa aliye na umri wa miaka 45 ambaye pia ni wakili na mhubiri, ameizindua kampeni hiyo katika mji wa Gweru, ulio kilomita 300 mashariki mwa Mji Mkuu Harare.

 Katika uchaguzi uliopangiwa kufanyikaAgosti 23, Chamisa atakuwa anapambana na rais aliye mamlakani, Emmerson Mnangagwa mwenye umri wa miaka 80.

Soma pia:Sheria tata ya "uzalendo" yaanza kutumika Zimbabwe

Mnangagwa amekuwa akikiongoza chama tawala cha ZANU-PF tangu mapinduzi yaliyomng'oa madarakani Robert Mugabe mwaka 2017.