1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Venezuela watafuta njia ya kuingia madarakani

31 Julai 2024

Upinzani nchini Venezuela unaodai ushindi katika uchaguzi wa urais nchini humo dhidi ya Rais Nicolas Maduro, unatafuta njia za kuingia madarakani licha ya vikwazo vikubwa vilivyopo.

https://p.dw.com/p/4iyPA
Kiongozi wa Upinzani Venezuela Maria Corina Machado na mgombea wa upinzani Edmundo Gonzalez
Kiongozi wa Upinzani nchini Venezuela Maria Corina Machado na mgombea wa upinzani Edmundo Gonzalez, wakiwahutubia waandamanaji baada ya matokeo ya uchaguzi kummpa ushindi rais Nicolas Maduro Picha: Leonardo Fernandez Viloria/REUTERS

Viongozi wa upinzani wanasema wameweza kufikia karibu 90% ya hesabu za kura ambazo kwa mujibu wa sheria zinapaswa kutolewa kwa mashahidi wakati wa kuhesabu kura, zinazoonesha kuwa mgombea wao Edmundo Gonzalez alishinda kwa zaidi ya mara mbili ya kura alizopata Maduro.

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umesema hautatambua matokeo ya uchaguzi wa Venezuela hadi rekodi zitakapothibitishwa.

Rais wa Venezuela aamuru jeshi na polisi kushika doria nchi nzima

"Walitangaza tu matokeo ya asilimia 80 ya kura bila ya kutoa chanzo chochote au mfumo ambao unaweza kuruhusu uhakiki wa matokeo haya. Na kwa matokeo haya yasiyoweza kuthibitishwa waliendelea kumtangaza Nicolas Maduro kuwa mshindi wa uchaguzi. Lakini sisi tumesisitiza kwamba uwazi na uadilifu wa mchakato wa uchaguzi lazima uhakikishwe," amesema mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Mataifa Josep Borrell.

Rais Maduro ametangaza ushindi na kukemea maandamano yaliyotokea kote nchini humo na kuyataja kuwa jaribio la mapinduzi.