1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Syria wasema Assad hana nafasi tena

31 Machi 2017

Upinzani wa Syria umesema hautokubali Rais Bashar al-Assad kuwa na dhima yoyote kwa mstakabali wa nchi hiyo ilioathirika na vita. Nayo Marekani imesema suala la kumuondowa Assad kwa wao sio tena kipau mbele

https://p.dw.com/p/2aTIM
Kasachstan Syrien Friedensgespräche in Astana Opposition
Picha: Reuters/M. Kholdorbekov

Yehia Aridi afisa katika kundi la Kuu la Mazungumzo la upinzani la NHC amesema Assad hakubaliki kamwe kama rais na kuongeza katika taarifa ya WhatsApp kwa shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba hakuna nchi itakayokubali kuwa na kiongozi alietenda uhlifu wa vita.

Matamshi hayo ya Aridi yanakuja kufuatia yale yaliyotolewa na balozi wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa Nikki Haley aliyesema kwamba kipau mbele cha serikali ya Marekani sio tena kukaa na kulenga juu ya namna ya kum'ngowa Assad.

Kauli hiyo ya Haley ni kuachana na sera ya utawala wa Obama ambayo mara kwa mara imekuwa ikidai kundoka kwa Assad na kuwaunga mkono waasi wanaopambana kumn'gowa.                                                                             

USA Nikki Haley UN-Sicherheitsrat
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki HaleyPicha: picture-alliance/AP Photo/R. Drew

Haley amewambia waandishi wa habari hapo Alhamisi Marekani italenga kushirikiana na nchi kama vile Uturuki na Urusi katika kutafuta suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa Syria ambao hivi sasa uko katika mwaka wake wa saba.

Wakati hayo yakijiri mazungumzo ya amani ya Syria yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa huko Geneva yametumbukia kwenye mzozo wa urasimu tokea kuanza kwake mwaka huu na hata wale wasiokata tamaa watakuwa na kibaruwa kigumu kutamka kwamba yanaelekea katika kufikia makubaliano kati ya pande hasimu

Nyuma ya pazia uvumi umekuwa katika suala moja unaokusudia kumzuwiya msuluhishi wao Staffan de Mistura kupiga hatua yoyote ile ya maendeleo kutokana na suali : Je yuko njiani kuindoka?

Wakati wanadilomasia wa mataifa ya magharibi wana shauku ya kumtaka abakie vyanzo vya habari vya Urusi vimekariri duru zisizotajwa zikisema muda wa Mistura unamalizika Ijumaa na kwamba atajiuzulu rasmi hapo mwezi wa Aprili kabla ya kuanza kwa duru mpya ya mazungumzo hapo mwezi wa Mei.

Bashar al-Assad Interview
Upinzani unasema Rais Assad sio sehemu ya mustakabali wa nchiPicha: Reuters

Repoti nyengine za Urusi zinasema nwanadiplomasia huyo mkongwe ambaye alitimiza miaka sabini hapo mwezi wa Januari ataendelea kubakia kwa miezi mengine sita zaidi.

Urusi ambayo ni mshirika wa karibu wa Rais Bashar al-Assad kwa kiasi kikubwa inaonekana kushikilia turufu katika mazungumzo hayo halikadhalika katika medani ya mapambano.Mwaka jana waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alimtuhumu Mistura kwa kuyahujumu mazungumzo hayo kabla ya kumuidhinsha tena.


Wanadiplomasia wanasema hawajuwi kile alicho nacho mawazoni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress aliyeingia madarakani Januari Mosi lakini jina la Sigrid Kaag mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa Lebanone linatajwa tajwa kuchukuwa nafasi yake.

Mwandishi : Mohamed Dahman /Reuters/dpa

Mwandishi :Mohammed Abdul-Rahman