1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Israel watowa wito kufikiwa makubaliano vita Gaza

4 Septemba 2024

Kiongozi wa upinzani nchini Israel Yair Lapid ametowa mwito wa kufikiwa makubaliano na kundi la Hamas kumaliza vita Ukanda wa Gaza na kuachiliwa huru mateka wanaoendelea kushikiliwa na wanamgambo hao wa Kipalestina.

https://p.dw.com/p/4kHMS
Israel | Kiongozi wa upinzani Yair Lapid
Kiongozi wa upinzani nchini Israel Yair Lapid.Picha: Ohad Zwigenberg/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Kadhalika kiongozi huyo wa upinzani amesisitiza mwito wake wa kutaka mabadiliko ya uongozi wa kisiasa nchini humo akisema kwamba vita vitaendelea ikiwa serikali ya sasa itaendelea kubakia madarakani.

Hata hivyo, kwa upande mwingine waziri anayehusika na usalama wa ndani Itamar Ben Gvir kutoka chama cha msimamo mkali wa mrengo wa kulia, cha Otzma Yehudit amesema anafanya juhudi za kuyazima mazungumzo ya sasa yasiyo ya moja kwa moja na kundi la Hamas, kuhusu usitishaji vita Gaza.

Soma pia:Ni kwa namna gani vita vya Gaza vinawaunganisha Uturuki na Misri?

Ben Gvir amesema Israel haipaswi kufanya mazungumzo na wauwaji.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW