1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Haki za binadamuJamhuri ya Kongo

Upanuzi migodi DRC wachochea ukiukwaji wa haki za binaadamu.

12 Septemba 2023

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International limesema upanuzi wa migodi ya shaba na Cobalt nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umechochea kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu.

https://p.dw.com/p/4WDh9
DR Kongo MONUSCO | Flüchtlingslager in Ituri
Sehemu ya makazi ya jamii ya watu wasio na kipato KongoPicha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

Katika ripoti yenye kurasa 98, shirika la Amnesty na lile la Kongo IBGDH yaligundua kuwajamii zinazoishi karibu na miji yenye migodi kama Kolwezi, hulazimishwa kuyahama makazi yao ili kupisha miradi hiyo.

Ripoti hiyo imesisitiza kuwa watu hao wanapaswa kunufaika na uchimbaji wa madini hayo.

Soma pia:Mabomu yagunduliwa yametegwa kwa watoto pacha DR Congo- UN

Katibu Mkuu wa Amnesty International Agnes Callamard amesema shirika hilo linatambua hitaji muhimula kuelekea kwenye matumizi ya nishati mbadala lakini linalenga kukomesha vitendo vya dhuluma dhidi ya raia wa Kongo.