UN:Tunahitahi msaada mara mbili zaidi kwa wasudani
4 Septemba 2023Shirika la Umoja huo la kuhudumia wakimbizi,UNHCR na mashirika mengine washirika wake,wametowa mwito wa kupatiwa dola bilioni 1 za kununua msaada wa mahitaji muhimu pamoja na kuwalinda watu zaidi ya milioni 1.8 wanaotarajiwa kuwasili katika nchi jirani na Sudan kufikiwa mwishoni mwa mwaka huu.
Soma pia:Jenerali AbdelFatah al Burhani wa Sudan yupo ziarani Sudan
Awali shirika hilo lilihitaji kupatiwa dola milioni 445, lakini kupitia taarifa iliyotolewa na mratibu wa shughuli zake katika kanda hiyo,Mamadou Duian Balde, shirika hilo limesema watu wanaowasili katika eneo la mpakani kutoka Sudan wanajikuta katika hali ngumu kutokana na kukosekana kwa huduma za kutosha, pamoja na miundo mbinu mibovu.
Mpaka sasa shirika hilo limepokea asilimia 19 tu ya dola bilioni 1 wanazohitaji kununua misaada muhimu ya kibinadamu,kama maji,chakula na malazi.