1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNRWA yangoja ripoti uhusika watumishi shambulio la Okt 7

6 Februari 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linasubiri ripoti ya awali kuhusu madai ya Israel kwamba baadhi ya wafanyikazi wake walihusika katika shambulio la Oktoba 7.

https://p.dw.com/p/4c6U6
Ukanda wa Gaza
Shirika la UNRWA limekuwa likitoa msaada mkubwa kwa wakimbizi wa KipalestinaPicha: picture alliance/dpa/APA/ZUMA Press Wire

Mwakilishi wa shirikisho hilo nchini Lebanon amesema ripoti hiyo itakuwa tayari mapema mwezi ujao.

Mwakilishi huyo Dorothee Klaud amewaambia waandishi wa habari mjini Beirut kuwa, wafadhili 19 wamesitisha msaada wa kifedha kwa shirika hilo la UNRWA kufuatia tuhuma zilizotolewa na Israel.

Israel imewatuhumu wafanyikazi 12 kati ya 13,000 katika ukanda wa Gaza kuhusika na shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na kundi la Hamas.

Madai hayo yametokea wakati Israel ikikabiliwa na kesi ya tuhuma za mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ katika  vita vyake ukanda wa Gaza, baada ya miaka mingi ya Israel kutaka shirika hilo livunjwe.

Ofisi ya uangalizi ya Umoja wa Mataifa inaendelea na uchunguzi wa madai yaliyotolewa na Israel.