Union kufanya mazoezi ya faragha ili kujiondoa mkiani
13 Novemba 2023Msimu uliopita Union ilimaliza katika nafasi ya nne, na msimu huu ilianza kwa kushinda mechi tatu za kwanza kabla ya kufikia hatua ya mechi 14 bila ushindi wowote katika mashindano yote ambapo wamecharazwa katika mechi 13.
Waliambulia poiti ya pekee wiki iliyopita kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya walipotoka sare 1-1 dhidi ya Napoli lakini matumaini yoyote ya kuimarika yalimalizika jana.
Soma pia: Union Berlin yaanza kwa kucharazwa katika mechi yao ya kwanza ya UEFA
Jumapili katika kichapo kikali cha mabao 4-0 kutoka kwa viongozi wa Bundesliga, Bayer Leverkusen.
Union ilishuka hadi nafasi ya mwisho kabisa kwenye jedwali huku kocha Urs Fischer akisema kwamba timu yake sasa itafanya mazoezi ya faragha ili kujenga azma za kisaikolojia ya kutaka ushindi tena.
"Lazima tuzungumzie mchezo wa Leverkusen, kuna kazi nyingi mbele yetu katika wiki hizi mbili," Fischer alisema.
Nahodha wa timu Christopher Trimmel alisema baada ya kushindwa dhidi ya Leverkusen kwamba kuna kibarua kigumu mbele yao.
"Tumekumbana na vichapo vingi sana. Lazima tuboreshe katika maeneo mengi, kama hatutaweza itakuwa vigumu kukaa katika nafasi za juu. Kucheza dhidi ya kushushwa daraja unahitaji mbinu tofauti ya mwili, akili tofauti," Trimmel alisema.
Fischer ameiongoza Union tangu 2018, bado anaungwa mkono na viongozi wa klabu, wachezaji na mashabiki, lakini mabadiliko yanahitajika na zimebaki mechi tano hadi mapumziko ya msimu wa baridi, Novemba 24 wanatarajia kuchuana na Augsburg.
Kisha wanamiadi na mabingwa Bayern Munich kabla ya kumaliza mwaka dhidi ya Borussia Mönchengladbach, halafu wapambane na timu nyengine zilizo mkiani Bochum na Cologne.