UNICEF yatoa hadhari ya kusambaa Kipindupindu nchini Kongo
19 Agosti 2023Matangazo
Kwenye taarifa yake, UNICEF inakadiria kwamba zaidi ya watoto 8,000 walio chini ya miaka mitano wameugua kipindupindu ndani ya mwaka huu, huku visa zaidi ya elfu 30,000 vya ugonjwa huo vikiripotiwa nchi nzima hadi kufikia sasa.
Mratibu mwandamizi wa dharura kutoka UNICEF aliyeko Goma, Shameza Abdulla amesema ikiwa hatua za haraka hazitochukuliwa ndani ya miezi ijayo, kuna kitisho kwamba ugonjwa huo utaenea katika maeneo mengine ya nchi ambayo yalikuwa bado hajayaathirika kwa miaka mingi.
Mwaka 2017 ugonjwa huo uliathiri maeneo mengi ya nchi, ikiwemo mji mkuu wa Kinshasa ambapo visa 55,000 na zaidi ya vifo 1,000 viliorodheshwa.