SiasaMali
UNICEF yalaani ongezeko la ukatili dhidi ya watoto, Sahel
30 Mei 2024Matangazo
Gilles Fagninou, mkurugenzi wa UNICEF katika kanda ya Afrika Magharibi na Kati, amesema katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2023, ukiukwaji mkubwa dhidi ya watoto katika eneo la kati la Sahel, uliongezeka kwa zaidi ya asilimia 70 ikilinganishwa na miezi mitatu ya awali.
Watoto walitumiwa kufanya mauaji
Fagninou ameongeza kuwa visa vingi vilihusisha kusajiliwa na kutumiwa kwa watoto katika makundi yenye silaha pamoja na kufanya mauaji.
Soma pia:Watoto milioni 1.8 wamekimbia makaazi yao ukanda wa Sahel
Afisa huyo wa UNICEF pia amesema ongezeko la kusikitisha la matukio ya kikatili katika eneo la kati la Sahel lazima likomeshwe ikiwa watoto watahitajika kutambua haki zao za kimsingi za maisha.