1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Unicef : Watoto milioni 400 wanakabiliwa na adhabu za vipigo

11 Juni 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF), limesema watoto wapatao milioni 400 walio chini ya umri wa miaka mitano wanakabiliwa na adhabu ya kupigwa pamoja na matatizo ya kisaikolojia.

https://p.dw.com/p/4gthF
UNICEF yasema watoto milioni 400 wanakabiliwa na adhabu za vipigo
UNICEF yasema watoto milioni 400 wanakabiliwa na adhabu za vipigoPicha: Nicolas Economou/NurPhoto/picture alliance

Shirika hilo limesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 60 ya wototo wote wa umri huo duniani kote wanaopitia mateso ikiwa pamoja na kudhalilishwa kwa kutolewa lugha zisizo na staha.

Makadirio mapya ya UNICEF yanaonyesha data zilizokusanwa kutoka katika nchi 100 kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka jana wa 2023, kuhusu adhabu za kimwili na za kisaikolojia kwa watoto zimeonesha kuwa licha ya nchi nyingi kupiga marufuku adhabu ya viboko kwa watoto lakini takriban watoto milioni 330 kati ya watoto milioni 400 bado wanakabiliwa na adhabu hizo.

Mkurugenzi wa UNICEF Catherine Russell amesema katika taarifa yake kwamba malezi yenye upendo kwa watoto na kuwa na muda kucheza nao kunaweza kuwaletea watoto furaha na pia kuwasaidia wajisikie salama, na hivyo kuwaweka katika nafasi nzuri ya kuongeza maarifa na kujenga ujuzi,katika kuufahamu vyema ulimwengu unaowazunguuka.