Katika Mbiu ya Mnyonge, Halima Gongo anawaangazia Wadegere, jamii iliyotoka nchini Ethiopia miaka ya tisini, tangu kuja kwao Kenya, watu wa jamii hiyo, wamekuwa wakiishi kwa kujificha kwani jamii wanazotangamana nazo zimewavika dosari ya imani potovu kwamba Wadegere wanaandamwa na laana ya ufukara maishani mwao.