Haki za binadamuAsia
UN yatoa wito kuokolewa Warohingya 185 bahari ya Hindi
24 Desemba 2023Matangazo
Msemaji wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Babar Baloch, alisema walio katika mashua hiyo ni wakimbizi wa Rohingya takriban 70 kati yao ni watoto na 88 ni wanawake na kuongeza kuwa kadhaa kati yao wanahofiwa kuwa katika hali mbaya huku mmoja akiripotiwa kufariki.
Maelfu ya Warohingya ambao wengi wao ni Waislamu na wanaopitia mateso makubwa nchini Myanmar, wanafanya safari hatari za baharini kutoka Myanmar na kambi za wakimbizi nchini Bangladesh kila mwaka wakijaribu kuelekea Malaysia ama Indonesia.
Soma pia:Takriban Warohingya 170 wamewasili Indonesia
Kwa mujibu wa UNHCR tangu mwaka uliopita zaidi ya watu 570, wakiwemo wakimbizi wa Rohingya, wameripotiwa kufariki au kupotea baharini katika safari hizo.