UN yataka dola bilioni 1 kukabili mzozo wa kiutu Ethiopia
16 Aprili 2024Matangazo
Umoja huo umeeleza kuwa zaidi ya watu milioni 21 katika taifa hilo la Pembe ya Afrika wanahitaji msaada, ikiwemo chakula.
Kongamano hilo la wafahdili ambalo limeandaliwa kufanyika jioni ya leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya, linatarajia kuchangisha dola bilioni moja kwa ajili ya misaada kwa miezi mitatu ijayo.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, jumla ya dola bilioni 3.24 zinahitajika mwaka huu pekee ikiwemo ya kuwasaidia wakimbizi wa ndani milioni nne.