UN yasema iko tayari kupeleka chakula katika eneo la Darfur
17 Agosti 2024Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, lilipongeza hatua hiyo na kusema ni muhimu katika harakati za kuokoa maisha.
Kufunguliwa kivuko cha Adre kutawezesha msaada kufikishwa Darfur
Msemaji wa shirika hilo la WFP nchini Sudan Leni Kinzli, amewaambia jana waandishi habari mjini Nairobi kwamba kufunguliwa kwa kivuko hicho cha Adre, ambacho ni muhimu kwa usambazaji wa misaada ya kibinadamu, kutawezesha kufikishwa misaada katika jimbo la Darfur linalokumbwa na migogoro nchini Sudan, ambako baa la njaa lilithibitishwa wiki mbili tu zilizopita.
Soma pia:Waasi wa Chad waushambulia mji wa Adre unaopakana na Darfur
Kinzli ameongeza kuwa malori mawili yakiwa na takriban tani 6,000 za chakula kwa ajili ya watu wapatao 500,000 yalikuwa yakipakiwa, ili kupelekwa katika maeneo ya Darfur, mara tu watakapopata kibali cha serikali.