UN yaonya, raia wa Tigray wanakabiliwa na kitisho cha njaa
26 Mei 2021Matangazo
Mkuu wa masuala ya kiutu na Mratibu wa msaada wa dharura Mark Lowcock amesema kuna kitisho kikubwa cha baa la njaa kama msaada hautaimarishwa katika miezi miwili ijayo.
Amesema asilimia 20 ya idadi ya watu wa Tigray wanakabiliwa na uhaba wa dharura wa chakula, na kuwa uharibifu na mashambulizi dhidi ya raia yanaendelea mpaka sasa katika eneo hilo.
soma zaidi: Marekani yaiwekea vikwazo Ethiopia na Eritrea
Ikiwa ni zaidi ya miezi sita baada ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy AHmed kuanzisha kile alichoita operesheni ya kasi ya kijeshi, mapigano na ukiukaji wa haki vimeendelea Tigray, ambako kitisho cha njaa kimekuwa kikilikabili kwa miezi kadhaa.