UN yaonya kuwa binadamu wanaathrika na janga la joto kali
26 Julai 2024Guterres amesema kuwa mabilioni ya watu wanakabiliwa na janga hilo la joto, huku viwango vya joto vikidizi nyuzi joto 50 kote duniani.
Kwa mujibu wa mtandao unaofuatilia sayari ya dunia na mazingira yake kwa manufaa ya raia wa Ulaya wa European Copernicus, Julai 21, 22 na 23 ni siku tatu zilizokuwa na joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa duniani kote, huku Julai 22 ikishikilia rekodi kwa viwango vya nyuzi joto 17.16.
Utafiti unaonesha ongezeko la joto duniani linaongezeka kwa kasi kubwa
Guterres alisisitiza wito wake kwa watu kupambana na kile alichokiita uraibu wa nishati ya visukuku na kusema kwa sasa mtazamo wao ni juu ya athari za joto kali, lakini haipaswi kusahaulika kwamba kuna dalili nyingine nyingi mbaya za mgogoro wa hali ya hewa kama vile vimbunga vikali zaidi, mafuriko na ukame.