UN: Wanawake, watoto wako hatarini katika vizuizi vya Libya
13 Oktoba 2021UNICEF imesema katika taarifa yake hapo jana, kwamba karibu wanawake 751 na watoto 255 walikuwa miongoni mwa maelfu ya wahamiaji na watafuta hifadhi waliokamatwa katika misako ya mjini Tripoli mwezi huu, na kuongeza kuwa watoto watoto wasioambatana na watu wazima na vichaga visivyopungua 30 ni miongoni mwa wanaoshikiliwa.
Taarifa ya shirika hilo imesema usalama na ustawi wa wanawake na watoto hao viko hatarini.
Mamlaka nchini Libya ziliendesha msako mkubwa mjini Tripoli, ukiwalenga hasa wahamiaji haramu mapema mwezi huu.
Shirika la hisani la Madaktari wasio na Mipaka, lilisema wahamiaji wasiopungua 5,000 na wakimbizi walikamatwa kupitia misako hiyo ya vurugu na kuzuwiwa katika mazingira duni.
Mtu mmoja aliripotiwa kuuawa na wengine 15 kujeruhiwa, kwa mujibu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya.