1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Vifo 745,000 vimetokona na kufanya kazi sana

17 Mei 2021

Utafiti wa Shirika la Afya duniani WHO, na la kazi duniani ILO unaonesha kufanya kazi kwa muda mwingi katika kipindi cha mwaka 2016, kumechangia vifo 745,000.

https://p.dw.com/p/3tTeh
Symbolbild Laptop Frau Home Office Erschöpfung Stress Zoom Meeting Fatigue
Picha: ROBIN UTRECHT/picture alliance

Katika utafiti weao huo, mashirika WHO na ILO kwa pamoja yanakadiria watu 398,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa kiharusi na 347,000 magonjwa ya moyo kwa 2016. Sababu ambao inaoneshwa ni kufanya kazi kwa muda mrefu kunakofikia masaa 55 kwa wiki.

Kati ya mwaka 2000 na 2016, idadi ya vifo vilivyotokana na magonjwa ya moyo kwa sababu ya kufanya kazi kwa muda mrefu vimeongezeka kwa asilimia 42, na kiharusu asilimia 19. Na mzigo mkubwa wa vifo hivyo kwa asilimia 72 wanaubeba wanaume. Maeneo ambayo yanatajwa kuwa na athari zaidi  kwa wafanyakazi wa umri wa kati au wazee ni Magharibi mwa Asia Pasifiki na ukanda wa Kusini-Mashariki mwa Asia.

Masaa ya kufanya kazi kwa unafuu yawe 35 hadi 40.

Profesa Jian Li mmoja kati wa maafisa waandamizi wa WHO, walioshiriki utafiti huo anasema "Tumebaini kwamba, kufanya kazi kwa masaa 55 au zaidi kwa wiki, kuonaongeza hatari ya kufa kwa magoinjwa haya ya moyo kwa asilimia 17, baada ya miaka 10. Hilo limejikita katika takwimu za washiriki 340,000 za makundi ya tafiti 22 tofauti duniani. Vilevile tumebaini kufanya kazi kwa masaa 55 au zaidi kwa wiki kuonaongeza hatari ya kupata kiharusi kwa asilimia 35."

Schweiz Genf | WHO Direktor Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom GhebreyesusPicha: Martial Trettini/KEYSTONE/picture alliance

Hitimisho la utafiti huo linasema kufanya kazi kwa masaa 55 au zaidi kwa wiki kunahusiana na asilimia 35 ya hatari ya kupata ugonjwa wa kiharusi na asilimia 17 ya kufa kutokana na maradhi ya moyo, ikilinganishwa na kufanya kazi kwa masaa 35 hadi 40.

Aidha utafiti huo umebaini kuuwa idadi ya watu wanaofanya kazi kwa muda mrefu inaongezeka duniani, na kwa sasa ipo katika asilimia 9, kwa zingatia la idadi jumla ya watu.

Tahadhari ya WHO katika kuwanusuru wafanyakazi.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema janga la Covid-19 kwa kiwango kikubwa limebadili mtindo wa ufanyaji kazi wa watu wengine. Ufanyaji kazi kwa njia ya simu umekuwa na nafasi kubwa kwa sasa katika maeneo mengi ya viwanda, kwa hivyo inakuwa kikwazo kati ya nyumbani na maeneo ya kazi.

Amesema hakuna kazi yoyote ambayo inatengwa na hatari ya magonjwa ya kiharusi na moyo na hivyo kuzitaka serikali, waajiri na wafanyakazi kufanya jitihada ya pamoja katika kukukubaliana muda wa kufanya kazi kwa shabaha ya kuzilinda afya za wafanyakazi.