UN: Urusi inatumia mateso ya kikatili nchini Ukraine
25 Septemba 2023Kulingana na Umoja wa Mataif, mifumo hiyo ni pamoja na kuwatesa wahanga hadi kifo. Mwenyekiti wa Tume hiyo Erik Møse ameliambia hii leo Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi.
Tume hiyo ilitembelea sehemu kadhaa za Ukraine zilizokuwa zikishikiliwa na vikosi vya Urusi hususan mikoa ya Kherson na Zaporizhzhia.
Na iligundua kuwa mateso hayo yalifanywa hasa katika magereza yaliyo chini ya udhibiti wa mamlaka ya Urusi na kwamba yanaweza kuchukuliwa kama uhalifu dhidi ya binaadamu.
Urusi ilipewa fursa ya kujibu madai hayo lakini haikuwa na mwakilishi katika kikao hicho. Moscow imekuwa ikikanusha mara kadhaa kufanya ukatili au kuwalenga raia katika vita vyake nchini Ukraine.
Makombora ya Urusi yamjeruhi mtu mmoja katika bandari ya Odessa nchini Ukraine