1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Mafuriko Sudan yazuia usambazaji wa misaada

9 Agosti 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema leo kuwa mafuriko nchini Sudan yamezuia usambazaji wa misaada katika maeneo mengi.

https://p.dw.com/p/4jIsI
Äthiopien I Überschwemmung in Süd-Godder, Amhara-Region
Picha: South Gondar zone Disaster prevention Office/Alemnew Mekonnen/DW

Maeneo hayo ambayo tayari yanakabiliwa na njaa, ni pamoja na kambi ya wakimbizi iliyoko Kaskazini mwa Darfur.

Katika taarifa yake, shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema takriban watu 11,000 nchini Sudan, ambao wengi wao wameyakimbia maakazi yao, wameathirika na mvua kubwa na mafuriko.

Sehemu kubwa ya nchi hiyo imeingia kwenye mgogoro wa kibinadamu tangu kuzuka kwa vita zaidi ya mwaka mmoja uliopita kati ya jeshi la Sudan na kundi la wanamgambo la RSF.

Baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na machafuko mabaya zaidi ni majimbo ya magharibi ya Darfur Kaskazini na Darfur. Ripoti ya shirika la usalama wa chakula IPC iliyotolewa mwezi uliopita imeonyesha kuwa sehemu za Darfur Kaskazini hasa kambi ya wakimbizi ya Zamzam inakabiliwa na hali mbaya zaidi ya njaa.