UN kupambana na homa ya mapafu na magonjwa ya kuharisha.
26 Aprili 2013Umoja wa mataifa umeanzisha kitengo maalumu cha kupambana na magonjwa ya homa ya mapafu na magonjwa ya kuharisha baada ya shirika la afya duniani (WHO), shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa (UNICEF), na kwa ushirikiano wa mashirika 100 yasiyo ya kiserikali, kuripoti kuwa magonjwa hayo yanasababisha vifo vingi vya watoto walio chini ya miaka mitano.
Kitengo hicho ambacho kitajulikana kama, mpango shirikishi wa kimataifa, wa kuzuia homa ya mapafu na kuharisha, kwa kifupi GAPPD, kimepewa kazi maalumu ya kupambana na magonjwa hayo duniani na kuhakikisha ya kuwa yawe ya mepungua kwa asiliamia 90 ifikapo mwaka 2025.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka mashirika hayo magonjwa ya homa ya mapafu na kuharisha, yamekuwa ya kichangia kwa 30% ya vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano duniani, ambapo ni sawa na watoto millioni mbili ambao hupoteza maisha yao kila mwaka, kutokana na kutopata huduma bora za afya.
Akiongelea kuhusu kuanzishwa kwa kitengo hicho maalumu, ambacho kitakuwa chini ya uangalizi wa umoja wa mataifa, Daktari Julio Frenk, ambaye ni mwalimu, wa maswala ya afya katika chuo kikuu cha Havard, amesema "kitengo hicho kitakuwa ni chombo muhimu kitakacho tumika katika kupambana magonjwa hayo, yanayo hatarisha maisha ya watoto, na kama kikitumika kwa ufasaha, basi kitaleta ushindi mkubwa sana katika jamii"
Mpango wa maji safi
Hata hivo Daktari Jennifar Cohn, ambaye anaongoza kampeni ya upatikanaji wa madawa kwa ajili ya shirika la madaktari wasio na mipaka, amesema kuwa, gharama za kawaida za matibabu kwa mtoto mmoja, zimepanda kwa asilimia 75 na ni jambo ambalo litaleta ugumu kwa baadhi ya nchi, na hasa zile zinazo tegemea misaada.
"Kwani ikitokea misaada hiyo kusimamishwa, basi lengo hilo la kutaka kuangamiza ugonjwa wa homa ya mapafu na magonjwa ya kuharisha huenda lisifikiwe."
Mchunguzi wa magonjwa ya kuharisha katika chuo kikuu cha Ghana, George Armah, ameliambia shirika la habari la IPS "ni muhimu kushughulikia magonjwa haya bila kutumia gharama kubwa,kwa kutoa kinga na kudhibiti maji taka katika mifereji na pia inatakiwa kubadili tabia na mienendo ya watu,kwani kinga pekee yake haitasaidia kupunguza magonjwa haya."
Mpango wa umoja wa mataifa wa kupambana ugonjwa wa homa ya mapafu na magonjwa ya kuharisha una ambatana sambamba na mpango wa shirika la kuhudumia watoto - UNICEF na wa shirika la afya dunia -WHO ambapo kwa pamoja yaliweka mkakati ya kuwa,ifikapo mwaka 2025 magonjwa haya yanayo hatarisha watoto, yawe yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Ikiwa hadi kufikia mwaka 2025, GAPPD itakuwa imefanikisha lengo lake la kupambana na magonjwa yanayo shambulia watoto wadogo, basi kitengo hicho, kuanzia mwaka 2030, kitapewa jukumu jingine la kuhakikisha ya kuwa kila mtu anapata huduma bora za afyana wakati huo huo maji safi yanakatika kila katika kila nyumba.
Na baadaye itakapofika mwaka 2040, GAPPD, itaongezewa jukumu jingine kwa kuhakikisha ya kuwa kila nyumba inakuwa na mfumo sahihi wa maji safi na maji taka.
Mwandishi: Rukundo Laurance/IPS
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman.