UN kufanya mkutano kuhusu teknolojia ya akili bandia.
17 Julai 2023Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza James Cleverly ataongoza majadiliano hayo ya kesho Jumanne.
Serikali kote ulimwenguni zinafikiria jinsi ya kupunguza athari za teknolojia ya akili bandia inayojitokeza, ambayo inaweza kubadilisha uchumi wa dunia na mazingira ya usalama wa kimataifa.
Soma pia:Jinsi gani serikali zitadhibiti teknolojia ya akili bandia?
Mnamo mwezi Juni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, aliunga mkono pendekezo lililotolewa na baadhi ya maafisa wakuu wa teknolojia ya akili bandia.
Pendekezo hilo lilihusu kuundwa kwa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi yake kama vile Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa, IAEA.