Zaidi ya wanawake, wasichana milioni 600 waathirika na vita
26 Oktoba 2024Maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa wamesema idadi hii ni ongezeko la asilimia 50 katika kipindi cha miaka 10.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema katika ripoti yake mpya kuwa maendeleo ya wanawake yanatoweka katikati ya viwango vya juu vya migogoro ya silaha na machafuko, na mafanikio yaliyoanza kuonekana ya haki za wanawake pia yako hatarini.
Ripoti hiyo imesema idadi ya wanawake waliouawa kwenye migogoro ya silaha imeongezeka mara mbili kwa mwaka 2023 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Katika mkutano wa siku mbili wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na suala hilo, Mkuu wa Shirika la Umoja huo la kuhamasisha usawa wa jinsia, ama UN Women, Sima Bahous aidha alisema sauti za wanawake katika michakato ya kutafuta amani hazizingatiwi.