UN: Hatari ya uhalifu wa kivita ni kubwa Gaza
6 Desemba 2023Volker Turk amesema kuna hatari kubwa ya kufanyika uhalifu mkubwa wa kivita katika mazingira ya aina hiyo ya kiwango cha maafa makubwa ya kibinaadamu.
Mkuu huyo wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa amesema watu milioni 1.9 kati ya milioni 2.2 wanaoshi katika ukanda huo wameyakimbia makaazi yao na wanaendelea kusukumwa katika maeneo yanayozidi kupungua yenye msongamano mkubwa wa watu kusini mwa Gaza katika mazingira machafu na yasiyo bora kwa afya.
Soma zaidi: Mzozo wa Gaza hauna mithili ukiangalia vifo vya wanahabari
Hayo yanajiri wakati wanajeshi wa Israel wakiendelea kukabiliana na wanamgambo wa Hamas huko Gaza baada ya kutanua operesheni yao ya mashambulizi ya ardhini hadi mji wa pili kwa ukubwa wa Khan Younis.
Hatua hiyo inaathiri pakubwa usambazaji wa msaada muhimu katika maeneo mengi ya ukanda huo.