UN - COP 25: Mazungumzo ya hali ya hewa yagonga mwamba
14 Desemba 2019Marekani, India, China na Brazil zimelaumiwa kwa kukosa muelekeo katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Mkutano wa mazingira wa COP 25 wa Umoja wa Mtaifa uliofanyika mjini Madrid, Uhispania na uliotarajiwa kumalizika jana Ijumaa, umeongezewa muda hadi leo Jumamosi ili kujadili zaidi masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Wawakilishi kutoka mataifa 200 wanakutana mjini Madrid kumalizia muongozo wa kuhusu hali ya hewa kwa mujibu wa mkataba wa Paris ea mwaka 2015, ambao unapendekeza upunguzaji wa joto la dunia hadikufikia kiwango cha chini ya digrii 2 Celsius.
Umoja wa Mataifa umesema ili kulipunguza joto kwa nyuzi 1.5 ulimwengu unahitaji kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa zaidi ya asilimia 7% kila mwaka hadi kufikia 2030. Wanasayansi wameonya kwamba dunia inakabiliwa na kasi isiyoweza kuzuilika ya ongezeko la joto duniani.
Kiwango cha joto duniani tayari kimeongezeka kwa nyuzi 1 Celsius, na kinaelekea kuongezeka kwa nyuzi zingine mbili au tatu ifikapo mwaka 2100.
Kwa mujibu wa wangalizi na wanadiplomasia, Marekani, ambayo haimo kwenye makubaliano ya Paris, imekuwa inazuia vikali marekebisho ya sheria ambayo yanaweza kusababisha nchi hiyyo pamoja na nchi zingine zilizoendelea kwenye ndoano ya kulipa fidia kutokana na uharibifu ghrama ambazo zinaweza kuzidi zaidi ya dola bilioni 150 kwa mwaka ifikapo 2025.
Mataifa ya ulimwengu yameshindwa kukubaliana mjini Madrid juu ya kufadhili mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa au kuhusu sheria zitakazosimamia ushirikiano wa kimataifa, na kutokukubaliana huko kunatokea kati ya nchi tajiri zilizo mstari wa mbele katika uchafuzi wa mazingira na mataifa yanayoendelea.
Vyanzo:/DPAE/AFP