Kituo cha Uongozi cha Julius Nyerere kilichoko kwenye chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda ni miongoni mwa vituo ambapo vijana wanapata fursa kuandaliwa kuwa viongozi kwa msingi wa kuzingatia falsafa za viongozi mashuhuri wa Afrika. Makala ya Vijana na Uongozi inakiangazia kituo hicho na umuhimu wake kwa vijana.