EU na Misri zaingia makubaliano biashara ya dola bilioni 1.1
29 Juni 2024Matangazo
Makubaliano hayo ya kifedha ni sehemu ya mwanzo ya ahadi katika kitita cha dola bilioni 4, ambacho Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen alikitangaza mwezi Machi.
Kwa mujibu wa halmashauri hiyo, fedha hizo zitatumika katika uwekezaji katika sekta kadhaa ikiwemo ya nishati safi. Mkataba huo umetiwa saini na Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya, Valdis Dombrovskis na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Misri Rania al-Mashat katika kongamano la siku mbili la uwekezaji la Umoja wa Ulaya na Misri la mjini Cairo.
Misri, ambayo inatoa hifadhi kwa takriban wakimbizi na wahamiaji milioni 9, inaathiriwa na vita vya miezi kadhaa kati ya Israel na Hamas katika eneo jirani la Ukanda wa Gaza.