UhamiajiEthiopia
Umoja wa Ulaya waweka masharti magumu ya visa kwa Ethiopia
29 Aprili 2024Matangazo
Hatua hiyo inafuatia kile umoja huo imekitaja kuwa ukosefu wa "ushirikiano wa kutosha" katika kuwarudisha nyumbani waomba hifadhi waliokataliwa pamoja na wahamiaji.
Hatua hiyo inamaanisha Waethiopia hawatatumia tena aina ya nyaraka wanazotoa ili kukidhi mahitaji ya maombi ya safari barani Ulaya. Hawawezi tena kupata visa ya kuingia Ulaya mara nyingi, na wanadiplomasia sasa watalazimika kulipa ada ili kupata visa.
Muda wa mchakato wa kupata visa pia umeongezwa hadi siku 45 kutoka siku 15. Sheria hizo ni sehemu ya mbinu ya Umoja wa Ulaya ya kudhibiti uhamiaji usio wa kawaida.
Umoja wa Ulaya uliweka taratibu kali kama hizo kwa Gambia.