1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya washutumu vitendo vya mateso Uganda

Lubega Emmanuel7 Februari 2022

Umoja wa Ulaya na Marekani zameshtumu hatua ya mwendelezo wa vitendo vya mateso na ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyofanywa  na vyombo vya usalama.

https://p.dw.com/p/46dre
Uganda Bereitschaftspolizei
Picha: Kasamani Isaac/AFP/GettyImages

Kanda ya video ikonyesha makovu yaliyojaa mgongoni mwa mwandishi Kakwenza Rukirabashaija imepokelewa na raia wa Uganda kwa hisia mseto za hasira, huzuni na huruma. Mwandishi huyo ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya mtandao kwa kumvunjia heshima rais Yoweri Museveni na mwanawe Jenerali Muhoozi Kainerugaba alikamatwa na kuzuiliwa kwa wiki kadhaa kabla ya kufikishwa mahakamani  na kisha kuachiwa kwa dhamana.

Lakini hii yote ilikuwa baada ya mwito na vilio kutoka ndani na nje ya Uganda mwandishi huyo wa vitabu viwili maarufu vya kisiasa aachiwe. Mwandishi huyo amesimulia hivi madhila yake akiwa mikononi mwa vyombo vya usalama.

Ujumbe wa Ulaya nchini Uganda umesambaza taarifa ukilaani vikali mienendo ya kuwatesa raia na pia kukiuka haki zao za kikatiba kwa kutowafikisha mbele ya sheria kwa wakati stahiki. Ujumbe huo umetaja vyombo vya usalama ikiwemo polisi na majeshi kwa kuwatisha na kuwahujumu raia pamoja na wanahabari kuwa mienendo ya kikatili siyostahili katika jamii iliyostarabika  na kudai kuzingatia utawala wa kidemokrasia.

Mahakama yatupilia mbali ombi la Kakwenza

Afrika | Kenia Uganda Proteste  Bobi Wine Opposition
Picha: AP Photo/picture alliance

Ujumbe huo umelezea kuwa mienendo hii ya kuwakamaka hasa wapinzani na wakosoaji wa utawala imendela tangu tarehe 18 mwezi Novemba mwaka 2020 katika kipindi cha kampeni za uchaguzi. Haya ni baadhi ya maoni ya watu kuhusu mienendo hiyo na shtuma za ujumbe wa Ulaya. Wiki moja baada ya kuachiwa, jamaa za Kakwenza walielezea yumo katika hali duni kiafya na anahitaji matibabu maalum nchini Ujerumani.

Ni kwa msingi huu ndipo wakili wake aliwasilisha ombi arudishiwe kibali chake cha usafiri. Hata hivyo alasiri ya leo mahakama imetupilia mbali ombi hilo kwa madai kuwa anaweza kutibiwa ndani ya nchi. Hadi wakati wa kuandaa taarifa hii, upande wa serikali haujajibu taarifa hiyo ya ujumbe wa Ulaya.