1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wasema ushindi wa Maduro hauwezi kutambulika

5 Agosti 2024

Umoja wa Ulaya umesema hapo jana kuwa ushindi wa rais wa Venezuela Nicolas Maduro katika uchaguzi wa mwezi uliopita unaozozaniwa hauwezi kutambulika.

https://p.dw.com/p/4j6eA
Venezuela l Nicolas Maduro
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro Picha: Matias Delacroix/AP/dpa/picture alliance

Umoja wa Ulaya umesema hapo jana kuwa ushindi wa rais wa Venezuela Nicolas Maduro katika uchaguzi wa mwezi uliopita unaozozaniwa hauwezi kutambulika, kutokana na Tume ya Uchaguzi kushindwa kutoa rekodi rasmi za matokeo ya upigaji kura.

Katika taarifa yake, Baraza la Umoja wa Ulaya limesema jaribio lolote la kuchelewesha uchapishaji kamili wa matokeo rasmi utazidisha mashaka juu ya uadilifu wa tume ya uchaguzi.

Tofauti na Marekani na nchi nyingine kadhaa, Umoja wa Ulaya umejizuia kumtambua mgombea wa upinzani Edmundo Gonzalez kama rais mteule.

Hata hivyo Umoja huo wa Ulaya umebainisha kwamba, kulingana na nakala za rekodi ya matokeo zilizochapishwa na upinzani na kupitiwa na mashirika kadhaa huru, zinaashiria kwamba mgombea huyo wa upinzani anaonekana kuwa alipata ushindi wa kura nyingi.