SiasaAsia
Umoja wa Ulaya waondoa vikwazo vya vyakula vya Japan
13 Julai 2023Matangazo
Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Ursula Von der Leyen, amefahamisha hayo leo mjini Brussels.
Katika taarifa yake Umoja wa Ulaya umesema kuondolewa vikwazo hiyvo kunatokana na matokeo chanya ya udhibiti uliuofanywa na idara za Japan kwenye vyakula hivyo.
Soma zaidi: Japan: Kesi ya uvujaji wa data yazua wasiwasi kuhusu wanasayansi wa kigeni
Vikwazo hivyo viliwekwa tangu kuharibiwa kinu cha nyukulia cha Fukushima kutokana na tetemeko la ardhi pamoja na mawimbi ya Tsunami.
Licha ya kuondolewa vikwazo hivyo Umoja wa Ulaya utaendelea kuvikagua vyakula vinavoagizwa kutoka Japan kuhakikisha vina kiwango cha mionzi kinachoruhusiwa.