1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wakosoa vizuizi dhidi ya balozi wake Niger

7 Septemba 2023

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Niger amewekewa vizuizi vya kutembea katika mji mkuu Niamey.

https://p.dw.com/p/4W2Ri
EU Politiker Josep Borrell
Picha: Olivier Matthys/AP Photo/picture alliance

Umoja wa Ulaya umekosoa vizuizi vya kutembea alivyowekewa balozi wake nchini Niger. Umoja huo umesema katika taarifa yake kwamba unalaani na kujutia vizuizi hivyo vya uhuru wa kutembea alivyowekewa balozi wake anayehudumu mjini Niamey siku ya Jumanne wiki hii alipokuwa njiani kuelekea ubalozi wa Ufaransa.

Taarifa hiyo imesema kwa mujibu wa mkataba wa Vienna wa mwaka 1961 balozi huyo wa Umoja wa Ulaya aliidhinishwa ipasavyo na kwa hivyo lazima aweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu kulingana na mkataba huo. Taarifa hiyo hata hivyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo la Jumanne.

Umoja wa Ulaya umelaani vikali mapinduzi ya Julai 26 yaliyomuondoa madarakani rais wa Niger aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia, Mohamed Bazoum. Umoja huo umesitisha msaada wa kifedha kwa Niger na unajiandaa kuwawekea vikwazo waliohusika na mapinduzi hayo.