Serikali ya Burundi imepokea kwa furaha hatua ya Umoja wa Ulaya ya kuondoa vikwazo vya kiuchumi vya tangu mwaka 2016. Rais Evariste Ndayishimiye amesema hatua hiyo ni ya busara, huku waziri wa mambo ya kigeni Albert Shingiro akisema kuondolewa vikwazo hivyo kutaruhusu kuimarishwa uhusiano kati ya Burundi na Umoja wa Ulaya. Isikilize ripoti yake Amida Issa kutoka Bujumbura.