Umoja wa Ulaya waidhinisha ushuru mkubwa kwa gari za China
4 Oktoba 2024Matangazo
Duru kutoka mjini Brussels zinasema mataifa 10 wanachama, yakiwemo Ufaransa, Italia na Poland, yameridhia kutozwa nyongeza ya hadi asilimia 35.5 ya ushuru kutoka viwango vya sasa vya asilimia 10 kwa magari yote ya umeme yanayoingizwa kutoka China.
Nchi tano za Umoja huo, zikiwemo Ujerumani na Hungary, zimepinga hatua hiyo zikitoa hadhari kwamba itachochea vita vya kibiashara na China, ambayo ni moja ya washirika muhimu wa kibiashara wa kanda hiyo.
Soma zaidi: Orban atahadharisha Ulaya, China zaelekea vita vya kiuchumi
Umoja wa Ulaya unaituhumu China kutoa ruzuku ya kuyasaidia makampuni yake ya kuunda magari, mwenendo ambao unapunguza ushindani na kuvidhoofisha viwanda vya mataifa ya Ulaya.