1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kuwachuja waomba hifadhi

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

Mawaziri kutoka katika mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wamesema ni muhimu kuwachunguza kwa kina wahamiaji na wasaka hifadhi na kuwaondoa wale wanaoonekana kuwa hatari kwa usalama.

https://p.dw.com/p/4XlEm
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell.
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell.Picha: FREDERICK FLORIN/AFP

Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Sheria walikutana siku ya Alkhamis (Oktoba 19) mjini Luxemburg kujadiliana hatua za kuchukua kufuatia mashambulio mabaya huko Brussels na Ufaransa kukiwa na kitisho cha usalama kinachohusishwa na mzozo wa Israel na Palestina.

Soma zaidi: Mawaziri wa Uhamiaji wa EU wakutana kujadili usalama, uhamiaji

Kamishna wa uhamiaji wa Umoja wa Ulaya, Ylva Johansson, alisema wanahitaji kuwa na ufanisi, kuziba mianya na kuwa wepesi wa kufanya maamuzi pamoja na kupokea matokeo.

Mkutano huo ulitazamiwa kuwa ni fursa kwa mawaziri hao kubadilishana mawazo ana kwa ana tangu shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na kundi la wapiganaji wa Palestina, Hamas, ambapo Israel imejibu kwa mashambulizi makubwa dhidi ya Ukanda wa Gaza.