1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kujadili malengo ya tabia nchi

23 Oktoba 2014

Umoja wa Ulaya unajivunia kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi wakati ukikabiliwa na mkutano wa malengo ya makubaliano ya tabia nchi.

https://p.dw.com/p/1DZyZ
Aluminiumfabrik in Estado do Para Brasilien
Picha: picture-alliance/dpa

Mkutano huo unaandaliwa wakati jumuiya hiyo ikiwa katika hatua za mwisho kutambulisha shabaha mpya ya tabia nchi ya mwaka 2030 licha ya kuwa viongozi watahitaji kuugomea mpango huo kwanza na kugawanyika katika hatua za utekelezaji.

Kwa mujibu wa Umoja wa Ulaya wapo tayari kwa mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi wenye mabishano wiki hii huku kukiwa na kutokuelewana juu ya namna ya uwajibikaji katika kupunguza uzalishaji wa joto jingi, kurutubisha vilivyotumika na kuongeza uhifadhi wa nishati.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakabiliwa na matatizo ya mgogoro wa kiuchumi Ulaya na janga la kimataifa la mripuko wa Ebola Afrika Magharibi katika siku mbili za mkutano utakaofanyika Brussells siku ya Alhamisi huku mazungumzo ya Tabia nchi yakitarajiwa kuwa na changamoto kubwa.

Kohlenlager in Indien ARCHIV 2012
Wafanyakazi wa migodi ya makaa ya mawe nchini IndiaPicha: picture-alliance/dpa/Jaipal Singh

Kwa muda mrefu Umoja wa Ulaya unatafuta namna ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na lengo ni kuwa na alama kabla ya makubaliano ya kimataifa yatakayofikiwa mjini Paris mwaka 2015 katika mkakati mpya wa tabia nchi.

Shinikizo kwa washirika

Nchi 28 washirika pia wapo katika shinikizo la kutafuta namna ya kupunguza utegemezi wa nishati kutoka Russia .Wanadiplomasia wanasema kunadhamira ya mpango wa mgomo siku ya Alhamisi katika mkutano wa malengo ya tabia nchi kwa mwaka 2030 ambao unamaana ya kusaidia kupunguza hewa ukaa, ambayo inaaminika kusababisha ongezeko la joto duniani lakini wanachama wa Umoja wa Ulaya bado wapo mbali na maelezo hayo.

Mwanadiplomasia mmoja kutoka Mashariki mwa Ulaya aliyekataa jina lake kujulikana alibainisha kuwa ni makubaliano magumu kwa mwaka huu huku Katibu wa Uingereza wa mabadiliko ya tabia nchi Edwad Davey hivi karibuni alisema wataenda kuweka mambo sawa na kama watashindwa watachekwa na Moscow na Moscow watasema Umoja wa Ulaya umegawanyika, ni dhaifu na upo katika mazingira magumu.

Viongozi wa ulaya wanatakiwa kuzingatia malengo matatu ya tabia nchi kwa mwaka 2030. Katika Tume ya Ulaya, watendaji wa jumuiya wanapendekeza kuhitaji kukata asilimia 40 ya uzalishaji wa gesi aina ya Carbondioxide, kwa kuzingatia viwango vya mwaka 1990.Pia Umoja wa Ulaya unapenda upatikanaji wa angalau asilimia 27 ya nishati inayotumika iwe ni kutoka katika vyanzo mbadala na kupunguza matumizi ya nishati kwa asilimia 30 ambapo kituo cha kutoelewana kipo katika namba hizo na ni lazima kuvifuata.

BdT Greenpeace Proteste in Berlin
Mwanaharakati wa mazingira mjini Berlin akipinga ongezeko la hewa ya Carbon DioxidePicha: AP

Malmaka ya lazima yanatarajiwa kuwa katika utoaji na urutubishaji wakati lengo la ufanisi wa nishati linauwezekano wa kutolewa taarifa wa namna ya nchi wanachama wanavyoweza kuamua.

Utata katika kufikia makubaliano

Nchi za Ulaya Mashariki zinatarajiwa kuwa na vita vikali katika mkutano huo huku wengi wao ni wenye kujitegemea katika matumizi ya nishati zinazochafua mazingira ambazo vyanzo vyake ni makaa ya mawe,wao wanahitaji msaada utakao wasaidia kufikia lengo la uzalishaji na wanaonyesha wasiwasi wa kufikia malengo kwa ufanisi. Kama anavyo onya Waziri Mkuu mpya wa Poland Ewa Kopacz kuwa serikali ya Poland haitakubaliana na masharti yoyote ambayo yanamaanisha gharama za ziada katika uchumi au bei ya juu ya nishati kwa walaji.

Uingereza nayo inajitenga dhidi ya malengo ya EU katika urutubishaji na ufanisi pamoja na Davey kusema kwamba nchi wanachama wanapaswa kubadilika wakati wa kuchagua namna ya kuondoa hewa ya cabon ambayo ni gharama kubwa Lakini wakati mwingine nchi kama Ujerumani wanataka kuwepo sheria ili kuhakikisha hayo yanatekelezwa katika bodi.

Rainer Baake katibu wa nishati kwa nchi wanachama anasema tukiwa na tamaa ya kupata makubwa katika malengo tutafanya mengi kwa ajili ya nishati, usalama, uwekezaji ugunduzi, na ajira za siku zijazo.

Wakati huo huo makundi ya mazingira yanautaka Umoja wa Ulaya kuwa na haja zaidi na mkakati wa Amani wa kijani kwa kutetea asilimia 55 ya kukata uzalishaji joto, asilimia 45 ya urutubishaji wa vilivyotumika na asilimia 40 ya uhifadhi wa nishati.

Mwandishi: Zuhura Hussein/DPA.

Mhariri: Josephat Charo.