Umoja wa Mataifa watoa tahadhari ya njaa inayoongezeka DRC
21 Septemba 2023Matangazo
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema mwaka huu nchini Kongo, takriban watu milioni 25.8 watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Msemaji wa WFP Tomson Phiri amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa kwamba kwa ujumla, wanahitaji dola milioni 870 ili kutoa misaada ya kibinadamu nchini DRC.
WFP: Njaa itaongezeka baada ya ufadhili kupungua
lakini amesema kwa sasa wamepungukiwa na asilimia 85 ya fedha hizo, ikiwa ni sawa na dola milioni 738.5.
Phiri amesema hali ni mbaya zaidi Mashariki mwa Kongo, sehemu inayokumbwa na mgogoro uliosahaulika.