Umoja wa Mataifa wataka dola milioni 371.4 kwa Lebanon
8 Januari 2025Matangazo
Ombi hilo ni baada ya lile la awali la dola milioni 426 la mwezi Oktoba, wakati vita vilipoanza baina ya pande hizo mbili na kusababisha maelfu ya Walebanon kukimbia makaazi yao.
Wakati huo, zilikusanywa dola milioni 250, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Soma zaidi: Kiongozi mpya Syria aahidi kuheshimu mamlaka ya Lebanon
Mratibu wa huduma za kibinaadamu za Umoja wa Mataifa, Imran Riza, amesema ingawa usitishaji mapigano unaleta matumaini, bado kuwa zaidi ya wakimbizi wa ndani 125,000 huku wengine kwa maelfu wakikabiliwa na ugumu wa kuanzisha upya maisha yao.
Fedha zinazoombwa sasa zinaelekezwa kuwasaidia wakimbizi milioni moja wa Kilebanon, Syria na Palestina walioathiriwa moja kwa moja na vita hivyo.