1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Zaidi ya Wasudan milioni 30 wanahitaji misaada

6 Januari 2025

Umoja wa Mataifa umesema hii leo kwamba zaidi ya watu milioni 30, na nusu yao wakiwa ni watoto, wanahitaji misaada nchini Sudan ambayo inakabiliwa na vita vikali kwa muda wa miezi ishirini sasa.

https://p.dw.com/p/4orsE
Chad, Adre | Flucht
Wanawake waliokimbia vita Sudan wamepumzika katika kambi ya wakimbizi huko Adre, Chad, Oktoba 5, 2024.Picha: Sam Mednick/AP

Umoja wa Mataifa umetoa mwito wa kupatikana kwa dola za kimarekani bilioni 4.2 ukilenga kuwasaidia watu milioni 20.9 kote nchini Sudan. Kwa mujibu wa Umoja huo, watu milioni 30.4 wanahitaji msaada katika nchi hiyo inayokabiliwa na "mgogoro wa kibinadamu usio na kifani". Mgogoro unaoendelea nchini Sudan umeitumbukiza nchi hiyo katika mzozo mkubwa wa kiuchumi. Tangu mwezi Aprili mwaka 2023, vita kati ya jeshi kuu la Sudan na kikosi cha (RSF) vimesababisha vifo vya maelfu ya watu. Wasudan milioni 11.5 wamegeuka wakimbizi wa ndani na wengine wameikimbia nchi.