Un yasema ulimwengu "unakwenda mrama" upunguzaji gesi ukaa
14 Novemba 2023Matangazo
Hayo yametajwa katika ripoti ya Umoja huo iliyochapishwa leo Jumanne ambayo inaonesha ahadi za mataifa duniani za kupunguza utoaji wa gesi chafuzi kwa mazingira bado ni ndogo.
Ripoti hiyo inasema jumla ya ahadi zote kutoka karibu mataifa 200 zitashuhudia utoaji wa gesi ukaa ukipungua kwa asilimia mbili pekee ifikapo mwaka 2030.
Soma pia: Mamilioni ya watu wapambana na ongezeko la Joto duniani
Wataalamu wanasema hicho ni kiwango kidogo mno ikilinganishwa na pendekezo la kupunguza asilimia 43 ya gesi chafuzi kuepusha kiwango cha joto kupanda zaidi ya nyuzi 1.5.
Kiwango hicho cha joto ndiyo kinatajwa na wasayansi kwamba alau kitainusuru sayari ya dunia na zilzala ya mabadiliko ya tabianchi.