MigogoroMamlaka ya Palestina
Umoja wa Mataifa wasema misaada inashindwa kufika Gaza
5 Januari 2024Matangazo
OCHA imeeleza kuwa, Umoja wa Mataifa na washirika wake hawajaweza kutoa misaada ya kibinadamu upande wa kaskazini mwa mto Wadi kwa siku nne mfululizo. Hali hiyo imetokana na mapigano yanayoendelea au hata njia za kufikia maeneo hayo kufungwa.
Mahitaji ya kimsingi ikiwemo dawa yanahitajika kaskazini mwa Gaza kwa watu wapatao 100,000.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya dharura limetoa wito wa ufikiaji haraka wa maeneo ya kaskazini mwa Gaza ambapo njia za kuelekea huko zimefungwa kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, idadi ya Wapalestina waliouawa katika mzozo huo imepindukia watu 22,000.