1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Mabadiliko ya tabia nchi ni kitisho cha afya

2 Novemba 2023

Umoja wa Mataifa umesema mabadiliko ya tabia nchi yameleta kitisho cha afya kutokana na ongezeko la majanga ya hali ya hewa, na joto la kupindukia.

https://p.dw.com/p/4YKQ4
Symbolbild Klimawandel | Kanada Überschwemmung in Chilliwack
Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa kunyesha CanadaPicha: Jesse Winter/REUTERS

Kupitia ripoti yake ya kila mwaka ya hali ya hewa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa WMO, sasa linataka kuwepo kwa mifumo bora ya kutoa tahadhari inayoweza kujumuishwa katika sera ya afya ya umma.

WMO inasema taarifa kuhusiana na hali ya hewa hazijumuishwi kikamilifu katika mipango ya huduma ya afya.

Hali mbaya ya hewa inasababisha pia maradhi kwa watoto na hata wazee kutokana na ongezeko la joto ama baridi kali

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema joto la kupindukia ni chanzo kikubwa cha vifo vinavyotokana na hali mbaya ya hewa, ila katika nchi zilizoathirika na kadhia hiyo, ni nusu tu ya wanaofanya maamuzi kuhusiana na masuala ya afya ndio wenye uwezo wa kupata huduma za tahadhari.

Kati ya mwaka 2000 na 2019 vifo vilivyosababishwa na joto vinakadiriwa vilikuwa 489,000 kwa mwaka.