Umoja wa Mataifa waongeza muda wa misaada Syria
10 Julai 2021Matangazo
Nyongeza hiyo ya miezi sita itafuatiwa na miezi mingine sita baada ya makubaliano kati ya Marekani na Urusi makubaliano ambayo Umoja wa Mataifa unasema yatatoa fursa ya misaada itakayookoa maisha ya watu milioni 3.4 wanaohitaji misaada ya chakula na kiutu.
Suala la misaada kupelekwa kaskazini magharibi mwa Idlib eneo ambalo limeshikiliwa na waasi, limekuwa kipau mbele cha Rais Biden na alilizungumzia katika mkutano wake wa kilele na Rais Vladimir Putin mwezi uliopita.