1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia yashutumiwa kwa mauaji

24 Aprili 2019

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu Michelle Bachelet ameilaani vikali hatua ya Saudi Arabia ya kutekeleza hukumu za kifo.

https://p.dw.com/p/3HL2C
Symbolbild Selbstmord
Picha: vkara - Fotolia.com

Saudia ilitekeleza jambo hilo kwa kuwakata vichwa watu 37 katika miji sita nchini humo.

Wizara ya usalama wa ndani ya Saudia ilisema watu hao ambao wote ni raia wa Saudi Arabia walinyongwa kwa kuhusishwa na ugaidi.

Na sasa Bachelet amesema anasikitishwa na kutofuatwa kwa sheria na utaratibu wa kimahakama kutokana na madai kuwa washukiwa walikiri kujihusisha na ugaidi baada ya kuteswa.

Ameutaka uongozi wa Saudi Arabia kuangazia upya sheria za kupambana na ugaidi na kusimamisha mauaji yaliyokuwa yamepangiwa kufanywa, yakiwemo ya watu watatu ambao bado wanakabiliwa na hukumu ya kifo.