UN yakubali kuisaidia Kongo kusafirishaji vifaa vya kura
16 Desemba 2023Matangazo
Barua kutoka kwa rais wa baraza hilo la usalama, imesema kwamba kwa kuzingatia umuhimu wa kuanza kwa haraka kuandaa msaada ambao Kongo imeomba, wanachama wa baraza hilo wanapanga kumfahamisha katibu mkuu wa Umoja huo kwamba kikosi hicho cha MONUSCO kimepewa idhini ya kutoa msaada huo kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi kama ilivyoomba na serikali ya Kongo.
Soma pia:Kikosi cha Afrika Mashariki chaanza kuondoka Kongo
Barua hiyo imeendelea kueleza kuwa msaada huo wa MONUSCO utatolewa kwa kiwango ambacho hakitaathiri uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya awali. Serikali ya Kongo imetaka kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa kuondoka nchini humo baada ya kuhudumu kwa takriban miaka 20, na kusema kuwa kimeshindwa kumaliza mapigano nchini humo.