Umoja wa Mataifa wahitaji dola bilioni 3 kwa ajili ya Sudan
17 Mei 2023Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa Shirika la Misaada yaKkiutu la Umoja wa Mataifa, Ramesh Rajasingham, amesema msaada huo pia utawasaidia zaidi ya watu milioni moja wanaotarajiwa kukimbilia nchi za karibu mwaka huu.
"Mahitaji nchini Sudan ni muhimu na yapo kila mahali kama unavyoweza kutarajia kutoka kwenye mapigano. Kunahitajika msaada wa kimatibabu, chakula, usafi, makaazi na mshtuko. Na pia tunapokea ripoti zenye kutia wasiwasi za ongezeko la udhalilishaji wa kingono huku wahanga wakiwa bila msaada." Alisema.
Soma zaidi: Sudan yageuka uwanja wa mapigano kwa wapiganaji wa kigeni
Mapigano nchini Sudan yamezidisha mzozo wa kiutu nchini humo ambapo kati ya dkila watu watatu, mmoja alikuwa anategemea misaada hata kabla mapigano.
Madaktari wanasema karibu watu elfu moja wamefariki dunia ndani na nje ya Khartoum pamoja na jimbo la Darfur.